Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2020

ASANTENI WATANZANIA KWA KUENDELEA KUONESHA IMANI KWA RAIS WETU MPENDWA JPM NI IMANI JUU YA IMANI, NI IMANI KWA MAENDELEO YANAYOONEKANA

Picha
   Fuatana Nami*Joseph Yona* Watanzania waendelea Kuonesha Imani Kubwa kwa RAIS WETU MPENDWA #JPM. Wasema TunduALissu Ni Mropokaji Hana Sera, hasemi atalifanyia nini Taifa amebaki kubwabwaja ya kuwafurahisha waliomtuma. Taifa letu linasonga MBELE, MAENDELEO yanayofanywa na JPM Yanaonekana hata kwa watoto. Lissu itakuwa ubongo wake kuna sehem haupo sawa  kwanza ukifuatlia kwa ukaribu speach zake hasemi atawafanyia nini wananchi endapo ataokota Urais Kama TLS yaani yeye ni kuropoka tu maneno ambayo hayana Mbele wala nyuma, yoote yaliyofanywa na serikali ya awam ya tano hayaoni huyo ni mwehu kabisa. Hata mapambano dhidi ya Korona hakuyaona Kuwa tumewazidi viongozi Woote Duniani. Hebu jiulize, JPM angekubali total lockdown wakati wa corona kama ilivyo Kenya leo hii wewe binafsi ungekuwa katika hali gani? Nchi za Ulaya, America, Afrika na Asia pamoja na WHO wote wamechukua msimamo wa Tanzania katika kukabiliana na corona. Raisi Maghufuli anastahili heshima na pongezi kati...

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO AGOSTI 13,2020

Picha
     

Maudhui ya Redio za Nje ni lazima Yapitie TCRA-Dkt.Mwakyembe

Picha
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika kituo cha redio cha Mashujaa Fm ya mkoani Lindi ambapo amefanya mahojiano maalum,na kushuhudia makombe iliyopata kituo hicho katika maonyesho ya Nanenane kwa miaka mitatu mfululizo tangu mwaka 2018,ambapo mbali na kutoa pongezi amewataka kufanya kazi kwa weledi na kufuata misingi ya taaluma ya habari na sheria za nchi. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Mkoa wa Lindi na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wakati wa ziara yake mkoani hapo ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) pamoja na kuzungumza na wadau wa sekta anazozisimamia mnamo Agosti 11,2020. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika kituo cha redio cha Mashujaa Fm ya mkoani Lindi ambapo amefanya mahojiano maalum,na kushuhudia makombe iliyopata kituo hicho katika maonyesho ya N...

Zitto tulia acha upotoshaji

Picha
Na Hamis Shimye SIASA za Tanzania kila kukicha zinaibua machizi wapya kwenye siasa na safari hii, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka na kuonyesha uchizi wake hadharani. Kitendo cha kuandika Twitter na kueneza habari ya uongo kuwa kuna mpango wa wagombea wa Urais wa vyama vya upinzani watakatwa sio jambo la ukweli na linapaswa kukemewa na wanasiasa wote. Anachokifanya Zitto ni mpango katika strategia ya siasa ya kutengeneza agenda ya kuleta wasiwasi kwenye jamii ili ione kuna uonevu mkubwa utakaowezwa kufanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) jambo ambalo si kweli hasa ikizingatie ndio kwanza vyama vinachukua fomu za kuwania uteuzi wa Urais. Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) inaendesha mambo yake kiutaratibu na haina shinikizo kutoka kwa mtawala au vyama vya siasa na ndio maana kila Chama kimepewa fomu hadharani tena na Mwenyekiti mwenyewe wa tume, Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage na hakuna chama kilichopewa fomu ya kificho. Anachofanya Zitto Kabwe sio s...

GEREZA ROMBO WAPATIWA MAFUNZO YA KUDHIBITI UGONJWA WA KIFUA KIKUU MAGEREZANI

Picha
 Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP. Hassan Mkwiche akiwasili leo Agosti 11, 2020 katika Gereza la Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro akiwa ameongozana na msafara wa Timu ya wataalam(hawapo pichani)kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya. Kushoto kwake ni Mkuu wa Gereza Rombo, ASP. Lucas Mboje.  Mkuu wa Gereza Rombo, ASP. Lucas Mboje akiwa ameongozana na Timu ya wataalam kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya ambao leo wameendesha Mafunzo ya kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu magerezani kwa maofisa na askari wa Gereza Rombo.  . Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP. Hassan Mkwiche(katikati) akitoa maelezo mafupi kabla ya kuwakaribisha wataalam kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya kutoa mafunzo ya kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu magerezani kwa maofisa na askari wa Gereza Rombo. Kulia ni Naibu Mkurugenzi kutoka  Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya...

HIZI NDIZO BEI MPYA ZA MBOLEA KWA MSIMU UJAO WA KILIMO

Picha
IMEELEZWA kuwa kwa mwaka 2020/2021  bei ya mbolea ya kupandia(DAP) kitaifa itauzwa kwa shilingi 55,573 kwa mfuko wa kilogramu 50 ikilinganishwa na msimu wa kilimo uliopita ambayo iliuzwa kwa shilingi 58,433. Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.    Kwa upande wa mbolea ya kukuzia (UREA) itauzwa kwa shilingi 48,070 kwa mfuko wa kilogramu 50 ikilinganishwa na shilingi 49386 ya msimu wa mwaka 2019/2020 ''Kwa hiyo kuanzia leo,nikianzia na mbolea ya DAP   kwa mkoa wa Arusha itakua shilingi 55356 ikilinganishwa na shilingi 58208 ya mwaka jana ambapo itakua imepungua kwa shilingi 2852 kwa mfuko wa kilo 50,"alisema Waziri. Alisema kwa mkoa wa Dodoma bei elekezi ni shilingi 53,925 ikilinganishwa na shilingi 56790  ya awali ambayo imepungua kwa shilingi 2,865. Kwa Dar es salaam bei elekezi itakuwa shilingi 48717 ikilinganishwa na msimu uliopita 51952 itakuwa...

SIMBACHAWENE AWATAKA WATANZANIA WANAOISHI NJE YA NCHI KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA

Picha
  Na Mwandishi Wetu   SERIKALI imetoa rai kwa watanzania wote wanaoishi nje ya nchi kuzingatia taratibu za kisheria zenye lengo la kuwalinda pamoja na kupata hati za kusafiri Nje ya Nchi. Akizungumza hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya kupinga biashara haramu ya usafirisha wa binadamu duniani, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema kuwa hakuna haja ya watanzania kurubuniwa na watu wenye nia mbaya wanaojitangaza kuwa na uwezo wa kuwatafutia kazi Nje ya Nchi au ndani ya Nchi bali utaratibu wa serikali ufuatwe. ‘’ Utaratibu rahisi ni kibali cha mzazi na serikali ya kijiji, anapotoka kuja mjini tunaweza tukajua na kumlinda katika kuangalia haki zake na kuangalia endapo atapata madhara yoyote, cha kushangaza watu wanaofanya kazi hiyo hawataki kufuata taratibu za kisheria ambazo zimewekwa na serikali’’ amesema Waziri Simbachawene. Waziri Simbachawene amewataka majirani, wanaposikia manyanyaso katika familia ...

IMEKULETEA VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO AGOSTI 12,2020

Picha
            MAGAZETI