HIZI NDIZO BEI MPYA ZA MBOLEA KWA MSIMU UJAO WA KILIMO
IMEELEZWA
kuwa kwa mwaka 2020/2021 bei ya mbolea ya kupandia(DAP) kitaifa
itauzwa kwa shilingi 55,573 kwa mfuko wa kilogramu 50 ikilinganishwa na
msimu wa kilimo uliopita ambayo iliuzwa kwa shilingi 58,433.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Kwa
upande wa mbolea ya kukuzia (UREA) itauzwa kwa shilingi 48,070 kwa mfuko
wa kilogramu 50 ikilinganishwa na shilingi 49386 ya msimu wa mwaka
2019/2020
''Kwa
hiyo kuanzia leo,nikianzia na mbolea ya DAP kwa mkoa wa Arusha itakua
shilingi 55356 ikilinganishwa na shilingi 58208 ya mwaka jana ambapo
itakua imepungua kwa shilingi 2852 kwa mfuko wa kilo 50,"alisema Waziri.
Alisema
kwa mkoa wa Dodoma bei elekezi ni shilingi 53,925 ikilinganishwa na
shilingi 56790 ya awali ambayo imepungua kwa shilingi 2,865.
Kwa Dar es salaam bei elekezi itakuwa shilingi 48717 ikilinganishwa na msimu uliopita 51952 itakuwa imepungua kwa shilingi 3235.
Geita bei elekezi itakuwa ni shilingi 58313 ikilinganishwa na bei ya mwaka jana 61138 itakuwa imepungua kwa shilingi 2825.
Kilimanjaro bei elekezi 54316 ikilinganishwa na 57178 ya msimu uliopita na hivyo itakuwa imepungua kwa shilingi 2816.
Mkoa
wa Mbeya bei elekezi itakuwa ni shilingi 59136 ikilinganishwa na bei
iliyopita shilingi 59136 itakuwa imepungya kwa shilingi.
Mkoa wa Songwe bei elekezi ni shilingi 57480 ikilinganishwa na msimu uliopita shilingi 60318.
"Bei
hizo ni bei elekezi za juu hivyo inatakiwa ieleweke kuwa hizo ndizo bei
za juu labda huko kijijini sana inaweza ikapanda kidogo ambapo ukichukua
kwa wastani Nchini nzima kwa ujumla mwaka jana bei elekezi ilikuwa ni
shilingi 58433 na kwa mwaka huu bei mpya ninazozitangaza ni wastani wa
shilingi 55573 ambapo ukichukua mkoa wa kagera ambao ndo mkoa ulio mbali
bei elekezi 591195 ukilinganisha na bei iliyopita ambapo ilikuwa
shilingi 62110,"
Alisema
kuwa bei ya mbolea ya kupandia imeshuka amesema unafuu huo uongeze
matumizi ya mbolea kufikia kiwango cha kimataifa kinachotakiwa lakini
pia kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara na yale ya chakula hivyo
nchi itakuwa na chakula cha kutosha.
Bei
elekezi kwa aina ya pili ya mbolea ya kukuzia(UREA) kwa mfuko wa kilo50
Arusha bei elekezi itakuwa ni shilingi 47,698 ukilinganisha na bei ya
msimu uliopita 48998,Dodoma bei elekezi itakuwa ni shilingi 46267
ukilinganisha na bei iliyopita ambayo ilikuwa ni shilingi 47633.
Na Geita ni shilingi 50,655 ukilinganisha na bei ya msimu uliopita ilikuwa ni shilingi 51820
Mbeya bei elekezi ni shilingi 48635 ukilinganisha na bei ya mwaka jana 49892
Mikoa yote mwaka jana wastani wa UREA ilikuwa 49386 na sasa 48070 ambapo imepungua kwa shilingi 1316.
Na bei
elekezi kwa mbolea zilizoingizwa na vyama vya ushirika kwa msimu huu
mfuko mmoja utakuwa ni shilingi Kwa DAP 50,000 kwa mfiko wa kilo 50.
Mbolea hiyo iwafikie wanachi palepale kwenye chama kwa bei hiyo,tofauti na wafanyabishara wengine wanaofikishia mikoani, kuhusu
UREA alisema bei elekezi kwa vyama vya ushirika itakuwa ni 43500
kutakuwa na unafuu mkubwa sana na unafuu huu unatokana kwamba kama
tungekuwa tunatumia vyama vya ushirika katika kuagiza mbolea hizi
wakulima wangepata mbolea kwa bei ya chini sana.
Ameviagiza
vyama vyote vya ushirika kutumia fulsa hii iliyopo na mazingira wezeshi
yaliyotengenezwa na serikali ya awami ya tano kuhakikisha wanaagiza
mbolea kwa pamoja ili waweze kuwahudumia wananchi wao vizuri.
Hata hivyo alisema kusingetokea maambukizi ya virusi vya Corona Duniani bei hizo zingeshuka zaidi.
Pia
alisema thamani ya shilingi nchini imeshuka na dola imepanda na hivyo
gharama ya kubadilisha dola kuwa kubwa ikiwekwa kwenye shilingi ya
Tanzania bei zinaongezeka zaidi.
Waziri
wa Kilimo, Japhet Hasunga akizungumza na wandishi wa habari jijini
Dodoma kuhusiana na bei mpya ya mbolea kwa Msimu mpya wa Kilimo wa
2020/21.
Mshirikishe mwenzako:
Maoni
Chapisha Maoni