GEREZA ROMBO WAPATIWA MAFUNZO YA KUDHIBITI UGONJWA WA KIFUA KIKUU MAGEREZANI
Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP. Hassan Mkwiche akiwasili
leo Agosti 11, 2020 katika Gereza la Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro
akiwa ameongozana na msafara wa Timu ya wataalam(hawapo pichani)kutoka
Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya. Kushoto kwake
ni Mkuu wa Gereza Rombo, ASP. Lucas Mboje.
Mkuu wa Gereza Rombo, ASP. Lucas Mboje akiwa ameongozana na Timu ya
wataalam kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya
Afya ambao leo wameendesha Mafunzo ya kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu
magerezani kwa maofisa na askari wa Gereza Rombo.
.
Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza, SACP. Hassan Mkwiche(katikati) akitoa
maelezo mafupi kabla ya kuwakaribisha wataalam kutoka Mpango wa Taifa wa
kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya kutoa mafunzo ya kudhibiti
ugonjwa wa kifua kikuu magerezani kwa maofisa na askari wa Gereza Rombo.
Kulia ni Naibu Mkurugenzi kutoka
Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya(kushoto) ni
Dkt. Wilbard Mhandiki.
Mtaalam kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Emmanuel Matechi akitoa historia ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa washiriki.
Maafisa na askari wa Gereza Rombo wakifuatilia mafunzo ya kudhibiti kifua kikuu magerezani.
Timu ya wataalam kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya wakifuatilia mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo ya kudhibiti kifua kikuu magerezani kutoka Gereza
Rombo wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam kutoka Mpango wa Taifa
wa kudhibiti Kifua Kikuu - Wizara ya Afya leo mara baada ya mafunzo
leo Agosti 11, 2020(Picha zote na Jeshi la Magereza).
Maoni
Chapisha Maoni