Zitto tulia acha upotoshaji



Na Hamis Shimye

SIASA za Tanzania kila kukicha zinaibua machizi wapya kwenye siasa na safari hii, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka na kuonyesha uchizi wake hadharani.

Kitendo cha kuandika Twitter na kueneza habari ya uongo kuwa kuna mpango wa wagombea wa Urais wa vyama vya upinzani watakatwa sio jambo la ukweli na linapaswa kukemewa na wanasiasa wote.

Anachokifanya Zitto ni mpango katika strategia ya siasa ya kutengeneza agenda ya kuleta wasiwasi kwenye jamii ili ione kuna uonevu mkubwa utakaowezwa kufanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) jambo ambalo si kweli hasa ikizingatie ndio kwanza vyama vinachukua fomu za kuwania uteuzi wa Urais.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) inaendesha mambo yake kiutaratibu na haina shinikizo kutoka kwa mtawala au vyama vya siasa na ndio maana kila Chama kimepewa fomu hadharani tena na Mwenyekiti mwenyewe wa tume, Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage na hakuna chama kilichopewa fomu ya kificho.

Anachofanya Zitto Kabwe sio siasa za ustaarabu na anapaswa kuchukuliwa hatua kwa kueleza alipopata hizo taarifa kwa kuwa huu ni uchochezi wa kiwango kikubwa hasa wakati huu wa uchaguzi mkuu ambao unakuwa na mambo mengi kwa wanasiasa kutumia fursa hiyo kuleta mpasuko kwa jamii.

Tume ya Uchaguzi ni chombo huru kilichoanzishwa mwaka 1993 chini ya ibara ya 74(1) ya Katiba ya nchi ya mwaka 1977. Ambako kwa tafsiri ya kawaida kiko huru na kinajiendesha kwa uwazi na kila mtanzania anashuhudia.

Zitto anapaswa kuona thamani na utu wa mtanzania ni bora na hichi anachofanya sio sahihi kwanza ni matumizi mabaya ya mtandao na pili anafanya uchochezi mkubwa ambao una madhara makubwa kwa taifa hapo baadae.

Embu chukulia mfano, kugombea Urais kuna sifa zake ambazo zimewekwa wazi kikatibu na endapo wagombea waliochukua fomu wakakosa hivyo vigezo anataka walazimishwe kuchaguliwa kuwa marais.

Katiba imeweka wazi sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais katika sheria ya 1992 Na. 4, ambazo zimeanisha sifa hizo. Sasa tujiulize Zitto anataka tuamini hata wasiokuwa na sifa zilizotajwa kikatiba wagombee tu Urais.

Huu ni wakati wa wanasiasa kuchunga ndimi zao hasa wanachosema kiwe na uhakika na si kuzusha taharuki na kuleta wasiwasi kwa umma kwa kuwa wanachofanya si sehemu ya kuleta Umoja bali wako kwa ajili ya mpasuko.

Uchaguzi ni kitendo kinachofanyika kila baada ya miaka mitano, Zitto anapaswa kuiona Tanzania ni bora na inayopaswa kuishi zaidi kwa miaka mingi ijayo kwa kulinda ndimi yake au mkono wake kwa kile anachokiandika kiwe na maslahi kwa taifa.

Uwakala wa mabeberu anaoufanya hauna faida kwa kuwa anataka kuibomoa nchi iliyomkuza na kumsomesha na ninaamini hata mwisho wa safari yake itakuwa Tanzania, hivyo asituharibie nchi yetu nzuri ambao wazee wetu waliipigania kwa nguvu kubwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

PROF.LIPUMBA ACHUKUA FOMU YA URAIS

TUNDU LISSU APOTEZA KUMBUKUMBU.