TUNDU LISSU APOTEZA KUMBUKUMBU.

Na Mwandishi wetu, Singida.


Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameonekana kukumbwa na Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu tangu aliporejea Nchini. Hali hii imeonekana hivi karibuni tangu aanze safari yake ya kuomba wadhamini.
Hali hiyo imejiidhirisha hapa mkoani Singida wakati alipokuwa akihutubia na kutoa taarifa za uongo kuhusu deni la taifa kinyume na takwimu za BOT kwakupoteza kumbukumbu akataja takwimu zisizo sahihi.

Pia Lissu ameonekana kituko mbele ya waananchi wa mkoa wa Singida mara baada ya kushindwa kutaja jina la Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbas na kumwita Mohamed Abbas huku akiwa kajiamini kama yuko sawa .
Wajuzi wa mambo na wataalamu wanasema hali hii ya kupoteza kumbukumbu imemkuta tu mara baada ya kutua nchini na kukutana na maendeleo makubwa ndani ya muda mfupi mara baada ya kutoka kwa mabeberu.

Lissu ambaye alishukia uwanja wa Kimataifa wa Terminal 3 na kujionea mabadiliko makubwa

yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano bado ameonekana mtaani akiropoka kuwa Rais John Pombe magufuli ajafanya kitu jambo ambalo watu wamesema kuwa mgombea huyu anatatizo la kusahau.

“uwezi kuwa mtu umeshuka katika uwanja wa kisasa na wafuasi wako wakaja kukupokea kisha hatua chache baadae unasema nchi yetu aijafanyiwa kitu basi huo utakuwa wendawazimu”alisema Bi Sophia Mkumbo.

Jambo ambalo kwa sasa limekuwa gumzo mtandaoni na kumuonyesha kuwa mgombea huyo ni mwendawazimu ni pale aliposhindwa kuchambua faida za Ndege nchini wakati jambo hili ni lakawaida ndiyo maana msanii wa Umri mdogo Mai Zumo kaamua kujitokeza kumueleza Tundu Lissu na wenzie wachache wenye matatizo ya Kumbukumbu umhimu wa ndege nchini.
Hali hii ndiyo sababu ya Wafuasi wa Lissu wameamua kukaa kimya.
mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

PROF.LIPUMBA ACHUKUA FOMU YA URAIS