NCCR MAGEUZI WAJITOSA URAIS WACHUKUA FOMU
Mgombea wa Urais ,Yeremia Kulwa Maganja akikabidhiwa Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha NCCR MAGEUZI katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Mgombea wa Urais ,Yeremia Kulwa Maganja wakionyesha Mikono juu wakiwa na Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha NCCR MAGEUZI katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 pamoja na Mgombea Mwenza Haji Ambar Khamis mara baada ya kuchukua Fomu hizo katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma.
Mgombea wa Urais ,Yeremia Kulwa Maganja kupitia Chama cha NCCR MAGEUZI katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 akisaini Kitabu mara baada ya kuchukua Fomu hizo za Kugombea Urais katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles.
Mgombea Mwenza kupitia Chama cha NCCR MAGEUZI Haji Ambar Khamis akisaini kitabu katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma.
Sehemu ya wafuasi wa chama cha NCCR MAGEUZI walipomsindikiza Mgombea wa Urais ,Yeremia Kulwa Maganja kupitia Chama cha NCCR MAGEUZI katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.
Maoni
Chapisha Maoni